MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024 TAZAMA HAPA


KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


TAMISEMI AJIRA ZA WALIMU 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura 2024/2025

Filed in Ajira, Habari, Makala, Michezo by on 02/07/2024 0 Comments
Share this Post

NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura 2024/2025

NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura 2024/2025, NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mwaka 2024/2025,NEC Timetable For Improvement Of Voter Register 2024/2025,NEC Selected Applicants NEC Jobs Tanzania 2024.

NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura 2024/2025

NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura 2024/2025, NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mwaka 2024/2025,NEC Timetable For Improvement Of Voter Register 2024/2025,NEC Selected Applicants NEC Jobs Tanzania 2024.

Uzinduzi wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika Jumamosi ya tarehe 20 Julai, 2024 Mkoani Kigoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).

Kuelekea Uzinduzi huo hii hapa ni Ratiba Kamili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kwa Mikoa yote Mwaka 2024/2025.

RATIBA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA MWAKA 2024/2025 DONWLOAD PDF

NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura 2024/2025, NEC Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mwaka 2024/2025,NEC Timetable For Improvement Of Voter Register 2024/2025,NEC Selected Applicants NEC Jobs Tanzania 2024.UBORESHAJI WA DAFTARI

Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya Uteuzi.

Wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: –

 1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
 2. Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025;
 3. Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine;
 4. Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari;
 5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
 6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika.

Watendaji wa Uandikishaji/ Uboreshaji

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na:-

 1. Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa;
 2. Maafisa Waandikishaji;
 3. Maafisa Waandikishaji Wasaidizi;
 4. Waandishi Wasaidizi; na
 5. Mwenyesha Kifaa cha Bayometriki

Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura

Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.

Wajibu/Majukumu ya Mawakala wa Uandikishaji

 1. Kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
 2. Kushirikiana na Waandishi Wasaidizi kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio na sifa.

Pamoja na majukumu tajwa, Mawakala wa Uboreshaji hawaruhusiwi kufanya yafuatayo:-

 1. Kuingilia shughuli za uendeshaji wa zoezi la Uboreshaji. Msimamizi wa kituo ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya nani anastahili kuandikishwa au kuboresha taarifa zake kwa mujibu wa Sheria.
 2. Kufanya kampeni za kisiasa katika kituo cha uandikishaji
 3. Kuorodhesha majina ya watu wanaojiandikisha.

Kiapo cha Kutunza Siri cha Mawakala wa Uandikishaji

Kila Wakala wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, ni lazima kula kiapo cha kutunza siri za taarifa za mwombaji au Mpiga Kura aliyeandikishwa. Wakala atakula kiapo mbele ya Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Wakala wa uandikishaji katika kituo cha kuandikisha Wapiga Kura hakuzuii utekelezaji wa majukumu ya Uandikishaji Wapiga Kura.

Watazamaji wa Uandikishaji

Kwa mujibu wa Kanuni za 46, 47, 48, 49, 50 na 51 (1) za Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024  Watazamaji wa ndani na kimataifa, wanaruhusiwa kutazama mchakato wa Uboreshaji utakavyofanyika katika vituo vya Uandikishaji.

Watazamaji wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutembelea vituo vya Uandikishaji, ni lazima waombe na kupatiwa idhini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Watazamaji.

Aidha, Watazamaji 24 watakaoruhusiwa na Tume watapewa barua za kuwatambulisha kwa Maafisa Waandikishaji na Mwongozo wa watazamaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume.

Maafisa Waandikishaji watatakiwa kuwapa barua za kuwatambulisha kwa Watendaji wa vituo ambavyo watavitembelea.

Aidha, Watazamaji wa Uandikishaji wa Wapiga Kura hawapaswi kutoa maelekezo kwa Mwandishi Msaidizi katika kituo husika.

Kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura

Kwa mujibu wa Kifungu vya 11 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:

 1. Kulikagua Daftari;
 2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
 3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
 4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali

Kifungu cha 27 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura. Kifungu cha 28 Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,  kinaweka utaratibu wa kuweka pingamizi. Mtu aliyewekewa pingamizi hutakiwa kupelekewa taarifa ili aweze kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba (7).

Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Mahakama itapaswa kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kupokea rufaa hiyo, uamuzi wa Mahakama ya Wilaya na iwapo aliyewekewa pingamizi hakubaliani na 25 maamuzi ya Afisa Mwandikishaji ya kuendelea kukataliwa kuwemo katika Daftari, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi Wilaya ndiyo utakuwa uamuzi wa mwisho na mtu hatoweza kukata rufaa katika Mahakama nyingine yoyote.

KWA HABARI ZAIDI DOWNLOAD APP YA NIJUZE HABARI HAPA


KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Share this Post

Tags: , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!