MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024 TAZAMA HAPA


KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


TAMISEMI AJIRA ZA WALIMU 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukoba July 09-2024

Filed in Ajira by on 09/07/2024 0 Comments
Share this Post

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukoba July 09-2024

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukoba July 09-2024

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukoba July 09-2024

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukoba July 09-2024, Tangazo La Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya Ya Bukoba 09-07-2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba amepokea kibali cha ajira mbadala chenye Kumb.Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Utawala Bora.

Anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 20 za Mtendaji wa Kijiji III kama inavyoonekana hapa chini:-

✅MTENDAJI WA KIJIJI III (NAFASI 20)

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI KIJIJI DARAJA LA III

 • Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
 • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa rai ana mali zao, kuwa mlinzi wa amani na.msimamizi wa utawala bora katika Kijiji
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji.
 • Kuwa katibu wa mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
 • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
 • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na
  kuongeza uzalishaji mali
 • Kuwa kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
 • Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Kijiji
 • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji
 • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
 • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukoba July 09-2024

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukoba July 09-2024

KAZI NA MAJUKUMU
Awe na Elimu ya kidato cha nne (Form IV) au cha sita (Form VI) aliefuzu mafunzo ya Astashahada (NTA – level 5) katika moja ya fani zifuatazo: – Utawala, Sheria, Maendeleo ya jamii, Sayansi ya Jamii, Usimamizi wa Fedha na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

 • Mwombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
 • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
  Mwanasheria/Wakili.
 • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
 • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
  katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa aajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
 • Waombaji aambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anawani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
  (referees) watatu wa kuaminika.
 • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti ya kuzaliwa, Kidato cha
  Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
 • Testmonials” “Provisional Results”. Statement of Results”, hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
 • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
 • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.CCA.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
 • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19, Julai, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu.

Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA,
S.L.P 491,
BUKOBA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment
Portal kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

KWA HABARI ZAIDI DOWNLOAD APP YA NIJUZE HABARI HAPA


KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Share this Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!