Usajili Michezo

SIMBA Waweka wazi Ishu ya Chama Kusaini Yanga

SIMBA Waweka wazi Ishu ya Chama Kusaini Yanga

SIMBA Waweka wazi Ishu ya Chama Kusaini Yanga

SIMBA Waweka wazi Ishu ya Chama Kusaini Yanga

SIMBA Waweka wazi Ishu ya Chama Kusaini Yanga, Msemaji wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa Mchezaji, Clatous Chama amemaliza mkataba na klabu hiyo na kwamba kinachoendelea sasa ni mazungumzo ya kutafuta namna ya kumuongezea mpya.

Ahmed amesema, kuwa endapo haitafanikiwa kumuongezea mkataba Chama, basi Simba itatafuta namna ya kuagana na kiungo huyo fundi.SIMBA Waweka wazi Ishu ya Chama Kusaini Yanga

“Hadi sasa mimi kama Msemaji bado sijapata uhalisia wa kipi kinaendelea kama ameongezewa mkataba au viongozi wameamua aondoke ama mazungumzo bado yanaendelea,” amesema Ahmed wakati akiwa mubashara akijibu maswali ya mashabiki kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Likishamalizika kwa ngazi ya juu, uongozi unanipa taarifa au watatoa taarifa na Wanasimba wapate kufahamu kipi kinaendelea juu ya Mwamba wa Lusaka. Tuwe wapole ndugu zangu hadi Jumatatu (Leo) tutajua kinachoendelea,” amesema Ahmed ambaye ni mtangazaji wa zamani wa RFA na Azam Media.

Aidha Ahmed amesema kuwa, endapo Simba itafanikiwa kumuongezea mkataba kiungo huyo, itakuwa ni kwa maslahi ya klabu hiyo na kama itaamua kutomuongezea mkataba mpya pia itakuwa kwa maslahi ya Klabu.

KWA HABARI ZAIDI DOWNLOAD APP YA NIJUZE HABARI HAPA


KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

About the author

Nijuze

Leave a Comment