Ajira

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Singida June 22-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Singida June 22-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Singida June 22-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida Leo Juni 22-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida June 2024. 

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Singida June 22-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Singida June 22-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida Leo Juni 22-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida June 2024.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA 22-06-2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida amepokea kibali cha utekelezaji wa Ajira mbadala katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa barua yenye Kumb. Na.FA.228/613/01/B/080 cha Tarehe 22/04/2024. Pamoja na kibali chenye Kumb Na.FA.228/613/01/C/039 cha Tarehe 21/05/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo, anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa nafasi zifuatazo.:-

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (Nafasi 01)

SIFA ZA MWOMBAJI

 • Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI)
 • Awe amefuzu mafunzo ya Astashahada/Cheti cha Technician certificate (‘NTA lever 5’) katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo-Dodoma au chuo
  chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI III

 • Afisa masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikli ya Kijiji;
 • Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora wa Kijiji;
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji;
 • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
 • Kutafsiri na kusimamia sera sheria na taratibu;
 • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
 • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika Kijiji ;
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
 • Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji;
 • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
 • Kusimamia utungaji wa sheria ndogondogo za Kijiji; na
 • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi ya Mishahara ya Serikali, yaani TGS B kwa mwezi .

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II (Nafasi 01)

SIFA ZA MWOMBAJI

 • Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) wenye
  Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.
 • Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za compyuta za ofisi kama vile:- Word,Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali

MAJUKUMU MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II

 • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;
 • Kupokea wageni na kuwasili shida zao na kuwaeleza wanapoweza
  kusaidiwa ;
 • Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matuokio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
 • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wajukumu ya kazi;
 • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
 • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinahusika.
 • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
 • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi; na

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi ya Mishahara ya Serikali, yaani TGS C kwa mwezi .

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

 • Muombaji awe ni Raia wa Tanzania na mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa walioko kazini Serikalini
 • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma .
 • Muombaji aambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria au Wakili.
 • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
 • Maombi yote yaambatane nakala ya Vyeti vya Taaluma, vyeti vya kidato cha Nne (IV na VI) na picha moja ya rangi katika barua ya maombi.
 • Waombaji wote waambatanishe nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa ambao hawana vitambulisho hivyo, namba za nida ziandikwe kwenye maelezo binafsi (CV).
 • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
 • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
 • Uwasilishwaji wa taarifa na sifa za kuvushi wahusika watachukuliwa hatua za kishera.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 03 Julai,2024

MUHIMU kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyiosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa
Mkurugenzi wa Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 27,
SINGIDA.

N:B Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kieletroniki wa Ajira( Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo:http://portal.ajira.go.tz/, (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sekretalieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tanagazo hii HAYATAFIKIRIWA

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF

KWA HABARI ZAIDI DOWNLOAD APP YA NIJUZE HABARI HAPA


KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

About the author

Nijuze

Leave a Comment