Ajira

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Nyanghwale 20-06-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Nyanghwale 20-06-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Nyang`hwale 20-06-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyang`hwale 20-06-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya Nyang`hwale Juni 20-2024.

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Nyang`hwale 20-06-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Nyanghwale 20-06-2024, Nafasi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Nyang`hwale 20-06-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyang`hwale 20-06-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya Nyang`hwale Juni 20-2024.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG`HWALE 20-06-2024

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang`hwale kupitia kibali cha ajira mbadala chenye
Kumb.Na.FA.228/613/01/C/019 cha tarehe 20 Mei, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira
mpya. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang`hwale anatangaza nafasi ya kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa ya kujaza nafasi
ilivyoorodheshwa katika tangazo hili: –

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI MOJA (01)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na elimu ya Kidato cha nne au cha sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) Katika moja wapo ya fani zifuatazo:

Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI

 • Afisa masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
 • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao,kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji;
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Mendeleo ya Kijiji;
 • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
 • Kutafsiri na kusimamia sera,sheria na taratibu;
 • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali;
 • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji;
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
 • Mwenyekiti wa kikao cha wataalaamu waliopo katika Kijiji;
 • Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
 • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji; na
 • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali ya TGS B kwa mwezi

MASHARTI KWA JUMLA

 • Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18
 • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
  Umma.
 • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe
  (E- mail address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa
  kuaminika.
 • “Provisional/Testimonials/Statement of results” na hati za matokeo za
  kidato cha nne na sita (form IV na VI result slip) HAVITAKUBALIWA.
 • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
 • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
 • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya
  nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
 • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
 • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa
  na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali
  kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
 • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA)
 • Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
 • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni jumatano tarehe 03 JULAI, 2024.

MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG`HWALE
S.L.P.352
NYANG`HWALE

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https:portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT HAPA

KWA HABARI ZAIDI DOWNLOAD APP YA NIJUZE HABARI HAPA


KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

About the author

Nijuze

Leave a Comment