Ajira TAMISEMI

HALMASHAURI Zenye Uhaba wa Walimu Kupewa Kipaumbele Ajira Mpya

HALMASHAURI Zenye Uhaba wa Walimu Kupewa Kipaumbele Ajira Mpya

HALMASHAURI Zenye Uhaba wa Walimu Kupewa Kipaumbele Ajira Mpya

HALMASHAURI Zenye Uhaba wa Walimu Kupewa Kipaumbele Ajira Mpya

HALMASHAURI Zenye Uhaba wa Walimu Kupewa Kipaumbele Ajira Mpya,Naibu Waziri, TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Zainabu Katimba (Mb) amesema kuwa katika Ajira mpya za Kada ya Ualimu zitakazotolewa hivi karibuni mgawanyo wa walimu hao utazingatia Halmashauri zenye uhaba wa walimu.

Mhe. Katimba ameyasema hayo katika mkutano wa 15 kikao cha 52 cha Bunge la Bajeti linaloendelea jijini Dodoa jana tarehe 24.06.2024.

Amesema kuwa kwa mwaka 2024/25 Serikali inatarajia kuajiri walimu elf kumi na mbili (12,000) wa shule za msingi na sekondari ambao wanatapangiwa vituo vya kazi hususani kwenye Halmashauri zenye upungufu wa walimu.

HALMASHAURI Zenye Uhaba wa Walimu Kupewa Kipaumbele Ajira MpyaAkijibu swali la Mbunge wa Tabora, Mhe.Mwakasaka, Katimba amesema kuwa Manispaa ya Tabora  ina upungufu wa walimu kwa shule za msingi na sekondari na katika awamu inayokuja, Manispaa ya Tabora itapata mgao huo wa walimu watakao ajiriwa.

Pia mgao huo utajali uwiano kwa kila mkoa, halmashauru na mahitaji ya nchi nzima itapata mgao huo wa walimu wapya watakao ajiriwa.

Aidha Mhe. Katimba amesisitiza kuwa halmashauri kufanya msawazo wa walimu kwa kupunguza walimu mjini na kuwapeleka vijijini ili kupunguza ukali wa upungufu wa walimu katika maeneo ya vijiji huku serikali ikiendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga nyumba na kuendelea kuboresha mazingira ya walimu.

Katimba amesema Katika mgao wa walimu watakao ajiriwa watazingatia halmashauri ambazo zina uhitaji wa walimu pia amesema wamepokea maoni na ushauri kwa kuwazingatia swala la walimu wanao jitolea ili waweze kupata ajira.

‘Ombi hilo limepokelewa na kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Utumishi tunaangalia namna nzuri ya utekeezaji wa swala hilo.

KWA HABARI ZAIDI DOWNLOAD APP YA NIJUZE HABARI HAPA


KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

About the author

Nijuze

Leave a Comment